Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMISS yalaani mapigano katika jimbo la Unity, Sudan Kusini

UNMISS yalaani mapigano katika jimbo la Unity, Sudan Kusini

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, umeelezea kutiwa hofu na kuibuka tena mapigano katika baadhi ya maeneo ya jimbo la Unity nchini Sudan Kusini mnamo Jumatatu Aprili 14.

UNMISS imelaani vikali uhasama huu ulioanzishwa tena, kama ukiukwaji mkubwa wa makubaliano ya kusitisha mapigano, ambayo yalitiwa saini na pande husika katika mzozo huo mjini Addis Ababa, Ethiopia mnamo Januari 23 2104.

Kwa mujibu wa UNMISS, mapigano hayo mapya yalizuka katika maeneo kadhaa magharibi na kaskazini magharibi mwa Bentiu, mji mkuu wa jimbo la Unity Jumatatu asubuhi, na ilipofika Jumanne, vikosi vya jeshi la SPLM vilivyoasi vilikuwa vimeuteka mji wa Bentiu na maeneo jirani. Mapigano hayo yamesebabisha idadi ya watu walolazimika kuhamia katika ua la UNMISS kupanda hadi zaidi ya 12,000 tangu Jumatatu.

Hali nchini Sudan Kusini imezungumziwa hapo jana na Kamishna wa Muungano wa Ulaya, EU kuhusu Ushirikiano wa kimataifa, masuala ya kibinadamu na ya dharura, kabla ya mkutano wake na Katibu Mkuu Ban Ki-Moon

“una hofu sana kuwa mapigano yanapoendelea na kufanya kuwafikia watu wanahitaji usaidizi kuwa mgumu, na mvua zinapokaribia kuanza kunyesha, huenda katika miezi michache ijayo tukashuhudia utapiamlo nchini Sudan Kusini”