Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola Milioni 274 zahitajika CAR kusaidia wakimbizi

Dola Milioni 274 zahitajika CAR kusaidia wakimbizi

Wakati ghasia zinaendelea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi UNHCR pamoja na mashirika 14 ya misaada ya kimataifa yametoa wito kwa wafadhili kusaidia wakimbizi nchini humo ambapo dola milioni 274 zinahitajika. Taarifa kamili na Priscilla Lecomte.

(TAARIFA YA PRISCILLA)

UNHCR inakadiria kuwepo kwa takriban watu 200,000 waliokimbia Jamhuri ya Afrika ya Kati na kutafuta hifadhi katika nchi jirani za Cameroon, Chad, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Kongo. Shirika hilo linategemea idadi hii kufika 362,000 ifikapo mwisho wa mwaka huu.

Wakimbizi hawa ambao wengi wao ni wanawake na watoto, wameathirika na njaa, huku wakijeruhiwa kwa risasi au panga. Wengine ni raia wa Kongo, Chad au Cameroun waliokuwa wakimbizi ndani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, na wanaotaka kurejea nchini mwao.

Kiasi hicho cha fedha ni kwa ajili ya kusajili wakimbizi, kuwajengea kambi, na kuwapa huduma za maji, chakula, elimu na vingenevyo, kwa mujibu wa UNHCR

Shirika hilo linategemea pia kuwepo kwa wakimbizi wa ndani zaidi ya 600,000 wanaokimbia vita na mashambulizi yanayolenga hasa jamii ya kiislamu hivi sasa baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea decemba mwaka 2012.

Wakati hayoa yakiendelea mwandishi wa radio ya Umoja wa Mataifa Jean Piere Ramazan aliyeko Jamhuri ya Afriak ya Kati, CAR amefanya ziara katika mji uitwao Bangassou kusini mashariki mwa CAR na kusema licha ya machafuko nchini humo mji huo umeimarisha mania na ni mfano wa kuigwa

( SAUTI RAMAZANI)