Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAIDS yamteua David Luiz kuwa balozi mwema

UNAIDS yamteua David Luiz kuwa balozi mwema

Mchezaji wa kimataifa wa Brazil na timu ya Chelsea David Luiz amteuliwa kuwa balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la mapambano dhidi ya Ukimwi UNAIDS.

David Luiz ambaye ni nahodha msaidizi wa timu ya taifa ya Brazil itakayokuwa mwenyeji wa mashindano ya kombe la dunia mwezi Juni, atafanya kazi ya kampeni na kuwafikia watu huku akiwaleta pamoja nyota mbalimbali wa kandanda kote duniani hususani vijana na kujielekeza katika kupinga ubaguzi, kujikinga na ukimwi pamoja na tiba kwa wanaoishi na virusi vya ukimwi.

Akizungumzia uteuzi huo David Luiz anasema

(SAUTI LUIZ)

"Ni heshima kubwa kuteuliwa kuwa balozi wa kimatiaf wa UNAIDS na nataka kutumia fursa hii kueneza ujumbe kuhusu ukimwi kote duniani."