Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalam wa haki za Binadamu akaribisha kuachiliwa kwa wakimbizi wa Eritrea nchini Djbouti

Mtaalam wa haki za Binadamu akaribisha kuachiliwa kwa wakimbizi wa Eritrea nchini Djbouti

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Eritrea, Sheila B. Keetharuth, amepongeza kuachiliwa huru leo kwa wakimbizi wa Eritrea na waomba hifadhi ambao walikuwa wamezuiliwa kwenye chuo cha mafunzo ya polisi cha Nagad nchini Djibouti, baadhi yao kwa zaidi ya muaka mitano.

Kufuatia juhudi za pamoja za Ofisi ya Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR na wahudumu wa mashirika ya umma, serikali ya Djibouti ilikubali kuwaachia huru wakimbizi wote na waomba hifafhi wa Eritrea mnamo siku ya Jumpaili, Aprili 13, 2014. Wafungwa wa Eritrea hawakujumuishwa katika hatua hii.

Bi Keetharuth ameelezea hofu yake kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu wa mara kwa mara nchini Eritrea, ambao ulisababisha mamia ya maelfu ya watu kuitoroka nchi yao na kukimbilia mustakhbali hatarishi na wasioujua.

Ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuwapa angalau hifadhi ya muda ya wakimbizi au ulinzi wakimbizi na waomba hifadhi wapatao 300, 000 kutoka Eritrea, kulingana na ahadi zao chini ya sheria ya kimataifa kuhusu wakimbizi na haki za binadamu.