Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchumi unaojali mazingira kuchangia kwa dola bilioni 45 katika uchumi wa Kenya

Uchumi unaojali mazingira kuchangia kwa dola bilioni 45 katika uchumi wa Kenya

Nchini Kenya, Shirika la Mpango wa Mazingira katika Umoja wa Mataifa, UNEP, limesema kwamba uchumi unaojali mazingira unaweza kuchangia kwa dola bilioni 45 katika ukuaji uchumi ifikapo mwaka 2030. Taarifa na Priscilla

Ripoti iliyozinduliwa leo na serikali ya Kenya pamoja ya UNEP, imezingatia jinsi ukuaji wa uchumi unaweza kuongezeka kutokana na uwekezaji katika teknolojia zisizo haribu mazingira. Kwa mujibu wa ripoti, mageuzi hayo yataongeza usalama wa chakula, mazingira safi, na utumiaji endelevu wa maliasili. Matumizi ya nishati pia yanatakiwa kupungua kwa kutumia nishati endelevu.

Ingawa Kenya ni moja ya nchi za Afrika ambapo uchumi unaojali mazingira umeshawekwa katika sera na mipango ya serikali, bado changamoto ni nyingi ili kutekeleza mageuzi hayo katika sekta zote za uchumi.

Changamoto zilizotajwa ni pamoja na kupunguza idadi ya magari yaliyopo barabarani na kuwezesha mifumo ya usafarishaji safi wa umma kama mabasi au magari ya umeme.

Mulei Muia ni mkurugenzi wa mawasiliano wizara ya mazingira nchini Kenya anasema hatu walizochukua

Kwa jumla, Shirika la UNEP limeiomba serikali ya Kenya iwekeze pesa zaidi katika miradi ya usafirishaji, viwanda na ukulima inayotumia teknolojia safi. Pia imeiomba serikali itengeneze sheria, viwango vya usafi, na mifumo ya ushuru itakayotoa msukumo kwa uwekezaji katika uchumi unaojali mazingira.