Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upotoshaji wa taarifa, uchochezi na propaganda Ukraine zikomeshwe: Ripoti

Upotoshaji wa taarifa, uchochezi na propaganda Ukraine zikomeshwe: Ripoti

Upotoshaji wa taarifa, propaganda na uchochezi nchini Ukraine vinapaswa kusitishwa mara moja ili kuepusha ongezeko la mvutano, imesema ripoti mpya ya ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo kama anavyoripoti Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Ripoti hiyo imewasilishwa na Gianni Magazeni, kutoka ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ikizingatia taarifa zilizokusanywa wakati wa ziara zilizofanywa na Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu haki za binadamu Ivan Šimonović na jopo la waangalazi wa haki za binadamu.

Mathalani Ukraine Mashariki ambako kunaishi idadi kubwa ya wananchi wenye asili ya Urusi hali bado ni mvutano na imetaka hatua za haraka zichukuliwe kurejesha imani ya wananchi wa jamii zote kwa serikali

Ripoti imetaka kuchunguzwa kwa matumizi ya nguvu kupita kiasi kulikofanyw ana polisi wa kikosi maalum huko Berkut na ukiukwaji wa haki kwa waandamanaji Maidan ili wahusika wafikishwe mbele ya sheria.

Kuhusu Crimea ambako Baraza Kuu lilisema kura ya maoni si halali, ripoti inazungumzia athari zinazoibuka kuhusu haki za binadamu ikiwemo kuanzishwa kwa uraia wa Urusi..

(Sauti ya Gianni)

“Kwenye suala la utaifa hususan wale ambao hawataki kubadili utaifa wao na inaweza kuwa na athari kwenye uwezo wa kupata huduma, haki ya ardhi na haki nyingine muhimu za kiraia na kisiasa.”