Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR, Ethiopia zasaidia wakimbizi kutoka Sudani Kusini

UNHCR, Ethiopia zasaidia wakimbizi kutoka Sudani Kusini

Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR kwa kushirikiana na serikali ya Ethiopia linahaha kuwasaidia wakimbizi kutoka Sudani Kusini wanaokadiriwa kuwa zaidi ya elfu 90 ambao wamekimbilia nchini humo kufuatia machafuko yanayoendelea nchini mwao.

(TAARIFA YA GRACE)

UNHCR inawajengea kambi mpya, kuwafikishia mahema na kuwahamishia nyanda za juu wakimbizi hao wakati huu ambapo msimu wa mvua unakaribia.

Hapo jana UNHCR ilisafirisha kwa njia ya ndege mahema ya dharura 4,000 na kutua katika uwanja wa ndege wa Gambella huku hii leo mahema mengine 400 yakitarajiwa kuwafikia wakimbizi walioko kilomita 125 kutoka mjini Gambella. Mahema mengine yanatarajiwa kuwasili kwa kutumia ndege nyingine sita hivi karibuni.

Mellissa Flaming ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI MELLISA)

"Wakimbizi wanaendela kuwasili kutoka Sudani Kusini katika eneo la Gambella kwa wastani wa watu 800 hadi 1000 kw asiku wengi wao wakipitia mpaka wa Pagak. Asilimai 95 kati yao ni wanawake na watoto kutoka jimboni Upper Nile Wna hofu, hawana chakula na hiki ndicho kilichowafanya wakimbie. Wanawake wengi wanasema wanaume wanalazimishwa kuingia vitani huku wengine wakiuwawa."