Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mauaji katika shambulio chini Nigeria

Ban alaani mauaji katika shambulio chini Nigeria

Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa Ban Kin Moon ameshtushwa na kusikitishwa na upotevu wa maisha ya watu katika shambulio la bomu kwenye kituo cha bus leo katika eneo liitwalo Nyanyan karibu na mji mkuu wa Nigeria Abuja.

Taarifa iliyotolewa na mseamji wa Katibu Mkuu imesema Bwana Ban ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao pamoja na majeruhi.

Katibu Mkuu amelaani vikali mauaji ya kiholela na vitendo vya ghasia vinavyofanywa na makundi yenye msimamo mkali. Amesema watekelezaji wa matukio haya na wale wanaoendela kutekeleza mengine kaskazini mashariki mwa nchi lazima wafiishwe katika vyombo vya sheria.