Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yasihi nchi kuimarisha hatua dhidi ya ugonjwa minyauko ya migomba aina ya TR4

FAO yasihi nchi kuimarisha hatua dhidi ya ugonjwa minyauko ya migomba aina ya TR4

Shirika la kilimo na chakula duniani, FAO limetaka hatua kuchukuliwa zaidi kudhibiti ugonjwa wa mnyauko wa migomba aina ya TR4 ambao sasa umeenea kutoka Asia, Mashariki ya Kati na Afrika na kutishia kipato cha wakulima wa zao hilo la nane kwa kutegemewa duniani.

Mtaalamu wa mimea wa FAO Fazil Dusunceli amesema hatua zisipochukuliwa sasa hali itakuwa mbaya zaidi huku akieleza jinsi ugonjwa huo unaotokana na fangasi unavyoenezwa.

(Sauti ya Dusunceli)

Dusunceli ameongeza kuwa ugonjwa huo unaweza kuzuilika hata kwa kukata migomba iliyodhurika na wanachofanya sasa ni kutoa elimu, kusaidia nchi kuandaa mikakati ya mafunzo akitolea mfano Australia ambayo ilichukua hatua na sasa ugonjwa huo umekoma na kilimo cha migomba kuendelea.