Mvua kubwa zinazonyesha DSM Tanzania zakata mawasiliano baina ya miji.

13 Aprili 2014

Serikali ya Tanzania imesema mabadiliko ya tabianchi pamoja na shughuli za kibinadamu zimesababisha kubomoka kwa tuta la daraja la mto Mpiji linalounganisha jiji la Dar es salaam na mji wa kitalii wa Bagamoyo ulioko mkoa wa Pwani.

Afisa wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Stella Vuzo alifika eneo hilo na kumkuta Katibu Mkuu Wizara ya ujenzi Mhandisi Musa Iyombe akishuhudia kipande cha barabara kinachouganisha daraja hilo lililozinduwa mwezi Februari mwaka 2005 kikiwa kimekatika.

(Sauti ya Katibu Mkuu)

Mmoja wa waathirika wa mvua hizo Felista Galikunisha mkazi wa Kimele huko Bagamoyo akaeleza hali ilivyokuwa.

(Sauti ya Felista)

Hata hivyo Mhandisi Iyombe amesema serikali inafanya kazi kutwa kucha kuhakiksha mawasiliano yanarejea kwenye maeneo hayo.