Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Brigedia Jenerali Ahamed Mohammed azungumzia MINUSCA, MONUSCO na UNAMID

Brigedia Jenerali Ahamed Mohammed azungumzia MINUSCA, MONUSCO na UNAMID

Operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa zinaendelea maeneo mbali mbali duniani ikiwemo barani Afrika. Majukumu ya kila operesheni yanategemea mazingira husika, lakini kubwa ni kulinda raia. Tarehe 10 Aprili Baraza la Usalama limeidhinisha Umoja wa Mataifa kubeba jukumu la ulinzi wa amani huko Jamhuri ya Afrika ya Kati. Baada ya hatua hiyo Assumpta Massoi wa Radio ya Umoja wa Mataifa alizungumza na Mnadhimu Mkuu wa ofisi ya Kijeshi ya Idara ya ulinzi wa amani ya Umoja wa Mataifa Brigedia Jenerali Ahamed Mohammed ambaye alieleza mambo kadhaa ikiwemo ujumbe huo mpya MINUSCA, halikadhalika MONUSCO na UNAMID. Kwanza anaanza kwa kuelezea hatua ya baraza la usalama.