Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jeshi la wanamaji wa Italia laokoa maelfu ya wakimbizi katika bahari ya Mediterranean

Jeshi la wanamaji wa Italia laokoa maelfu ya wakimbizi katika bahari ya Mediterranean

Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR linakadiria kuwa takribani watu 6000 wameokolewa na jeshi la wanamaji wa Italia katika boti zaidi ya 40 ambazo zilijaza abiria kupita uwezo wake katika mwambao wa Sicily na Calabria katika bahari ya Mediterranean katika siku nne zilizopita

Kwa mujibu waUHNCR idadi kubwa ya watu hao ni watoto na wanawake, wengi wa watoto wakiwa ni wachanganga na wasio na walezi .UNHCR inasema watu hao walikuwa wanakimbi machafuko na waliondokea katika mji uitwao Zwara nchini Libya. Wengi hao wanatoka Syria, Eritrea, Somalia, Nigeria, Gambia, Mali na Senegal. Melissa Flaming ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI MELISSA)

Pia manusura wametuambia kuwa kuna maelfu ya wakimbizi wa Syria walioko Somalia wako Libya wanasubiri kuondoka, na wako katika mazingia ya kunyanyaswa kwani wamesafirishwa kimagendo na wanalipa zaidi ya dola elfu tano kwa safari hii.Tunaendelea kuzitaka nchi mbalimbali kufanya kazi pamoja kauokoa watu katika bahari kama jeshi la wanamaji wa Italia linavyofanya na pia kutunga sheria zitakazouia watu kufanya safari hizi za hatar