Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania yaeleza mikakati ya kudhibiti ajali za barabarani

Tanzania yaeleza mikakati ya kudhibiti ajali za barabarani

Hapo jana baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio lenye lengo la kuimarisha usalama barabarani na kuzitaka nchi wanachama kushughulikia tatizo la usalama barabarani kwa kupitisha mifumo sahihi ya udhibiti wa ajali na kuimarisha usalama barabarani .

Takwimu za shirika la msalaba mwekundu zinaonyesha kuwa watu 3,000 hufariki dunia kila siku kutokana na ajali za barabarani huku shirika la afya ulimwenguni WHO likisem aasilimia 80 ya vifo hivyo ni katika nchi za vipato vya kati ambako ni nusu ya magari yaliyosajiliwa duniani yanaendeshwa au kumilikiwa.

Mohamed Mpinga ni mkuu wa kikosi cha usalama barabarani nchini Tanzanaia na hapa anazungumzia mikakati ya kudhibiti ajali za barabarani.

(SAUTI MPINGA)

Kwa mujibu wa takwimu za WHO watu milioni moja walifarikia dunia kwa ajali za barabarani mwaka 2010 pekee.