Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya watoto walio na utapiamlo huenda ikaongezeka maradufu:UNICEF

Idadi ya watoto walio na utapiamlo huenda ikaongezeka maradufu:UNICEF

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa duniani UNICEF limeonya kwamba watoto wachanga katika taifa changa kabisa, Sudan kusini wako katika hatari ya kukabiliwa na hali mbaya ya lishe huku takriban watoto robo milioni wakitabirwa kukubwa na utapiamlo uliokithiri ifikapo mwishoni mwa mwaka huu iwapo hatua hazitachukuliwa.

Tangu nchi hiyo ipate uhuru mwaka 2011, inaelezwa kuwa idadi kubwa ya watoto nchini humo wanakabiliwa na uhaba wa lishe.

UNICEF imesema kwamba mapigano yanayoendelea yanahatarisha upatikanaji wa chakula na iwapo huduma ya tiba haitaimarishwa takriban watoto 50,000 walio chini ya umri wa miaka mitano huenda wakafariki dunia.

Kwa sasa zaidi ya watu milioni 3.7 wakiwemo watoto 740,00 walio na umri wa chini ya miaka mitano nchini humo wako katika hatari ya usalama wa chakula huku wengi wakiamua kula nyasi.