UNHCR yasambaza misaada ya kibinadamu Syria katika hali ya tahadhari

9 Aprili 2014

Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la wakimbizi UNHRC na lile la hilali nyekundi nchiniSyriakwa mara ya kwanza limefikisha huduma za kibinadamu kwa mamia ya wakazi wa Boustan al Qaser mashariki mwa mji wa Aleppo.George Njogopa na taarifa kamili.

(Taarifa ya George)

Magari mawili yakiwa yamebeba vifaa mbalimbali ikiwemo mablanketi, vyakula na mahiyaji mengine yaliwasili kwenye kituo cha mwisho cha ukaguzi na baadaye mizigo hiyo ilisafirishwa hadi katika maeneo yaliyopo karibu na mji waAleppotayari kwa kugawiwa kwa wananchi.

Kulikuwa na hali ya utulivu wakati wote wa operesheni ya uzambazaji wa misaada hiyo ya kibinadamu na hiyo ilitokana na pande zote kuafiki kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano wakati huu wa usambazwaji wa mahitaji hayo.

Mafisa wa UNHCR ambao waliendesha tathmini katika mji waAleppowalisema kuwa maeneo mengi yanakabiliwa na upungufu wa mahitaji muhimu ikiwemo chakula, maji na madawa.

Licha ya kwamba tathmini hiyo kwa mara ya mwisho ilifanywa Juni 2013, lakini maeneo hayo hayakufikiwa na huduma zozote mpaka zile zilisofarishwa mara hii.