WHO yatoa mwongozo wa tiba dhidi ya homa ya ini, Hepatitis C

9 Aprili 2014

Kwa mara ya kwanza kabisa Shirika la afya ulimwenguni, WHO limetoa mwongozo wa tiba dhidi ya ugonjwa wa homa ya ini, Hepatitis C, ugonjwa sugu ambao husababisha vifo vya  kati ya watu Laki Tatu Na Nusu  hadi Nusu milioni Kila mwaka. WHO inasema mwongozo huo umezingatia tathmini ya kina na ushahidi wa kisayansi kwa hiyo watashirikiana na serikali kujumuisha muongozo huo katika mipango ya tiba ya kitaifa. Taarifa kamaili na Joseph Msami

(TAARIFA YA MSAMI)

Taarifa iliyotolewa leo na shirika hilo imesema vifo hivyo ni miongoni mwa wagonjwa kati ya Milioni 130 hadi Milioni 150 ambapo mwongozo mpya  utarahisisha upatikanaji kwa urahisi wa dawa bora zaidi za kunywa na hata uwezekano wa kupata dawa mpya zaidi miaka michache ijayo.

Mwongozo huo una vipengele muhimu tisa ikiwemo kuongeza idadi ya wanaochunguzwa dhidi ya Hepatitis C, ushauri wa kupunguza kiwango cha ini kuharibika na kuchagua tiba sahihi pamoja na kinga.

WHO inasema kwa kufanya hivyo nchi zitaweza kuboresha utoaji wa tiba na huduma kwa wagonjwa wa homa ya ini na hivyo kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na saratani ya ini na kunyauka kwa ini.

Hali ya ugonjwa huu ikoje nchini Tanzania? Dk Vida Makundi ni mtaalamu wa ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa

(SAUTI VIDA 1)

Na je Muongozo huu wa WHO utaleta matumaini gani?

(SAUTI VIDA 2)