Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muarobaini wa upangaji miji ni mfumo shirikishi : Mshiriki mkutano wa makazi ya miji Colombia

Muarobaini wa upangaji miji ni mfumo shirikishi : Mshiriki mkutano wa makazi ya miji Colombia

Kongamano la Saba kuhusu makazi ya miji linaendelea mjini Medellin, Colombia, likiwa limeng'oa nanga . Maelfu ya watu wanashiriki kongamano hilo, kwenye mji ambao umeshuhudia mabadiliko makubwa katika kipindi cha takriban miaka 20, na kujikwamua kutoka katika umaskini, miundo mbinu duni, uhalifu na machafuko na kuwa mji wa kisasa.

Miongoni mwa watu wanaoshiriki kongamano hilo ni viongozi wa mabaraza ya miji au wale wanaohusika na maendeleo ya miji akiwamo Meja Mstaafu Suleiman Sumba, Waziri wa Mashamba, Upangaji wa miji, Nyumba na Ustawi, katika jimbo la Kakamega, nchini Kenya. Katika mahojiano maalum na Joshua Mmali wa idhaa hii Bwana Sumba anasema muarobaini wa kufanikisha upangaji miji ni kuwshirikisha wananchi na kuachana na mfumo wa kufanya muumuzi yasiyo shirikishi.

Kwanza anaanza kueleza adhma ya serikali ya Kenya katika kukuza miji

(SAUTI SUMBA)