Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuna hofu na kinachoendelea Burundi: Baraza la Usalama

Tuna hofu na kinachoendelea Burundi: Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeeleza wasiwasi wake na kile kinachoendelea Burundi wakati huu ambapo nchi hiyo inajiandaa kwa uchaguzi mkuu mwakani.

Hiyo ni kwa mujibu wa Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Balozi Balozi Joy Ogwu, alipozungumza na waandishi wa habari baada ya mashauriano ya faragha ya wajumbe, ambapo walipokea ripoti kutoka kwa Mkuu wa masuala ya siasa ndani ya Umoja huo Jeffrey Feltman.

Feltman aliwaeleza wajumbe uwepo wa changamoto za kiusalama kutokana na ghasia zinazosababishwa na vijana wafuasi wa vyama vya siasa nchini humo. Kwa mantiki hiyo wajumbe wamesema..

(Sauti ya Balozi)

“Sote tumeelezea wasiwasi wetu kutokana na ghasia zinazoendelea nchini Burundi wakati huu nchi hiyo inakaribia uchaguzi mwaka 2015. Tumerejelea wito wetu wa mashauriano shirikishi kwa wadau wote  kwa maslahi ya amani na utulivu Burundi. Na bila shaka, msingi wa kuendeleza mashauriano na maridhiano ni makubaliano ya Arusha.”