Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana lazima wapewe kipaumbele ili kuondoa umaskini: Chissano

Vijana lazima wapewe kipaumbele ili kuondoa umaskini: Chissano

Changamoto ya ajira kwa vijana lazima ishughulikiwe kwa kasi katika kusongesha juhudi za kupambana na umaskini hususani barani Afrika amesema rais msataafu wa Msumbiji Joaqium Chissano ambaye ni miongoni mwa wenyeviti wa mkutano wa kamisheni ya watu na maendeleo unaojadili utekelezaji wa makubaliano ya Cairo miaka 20 iliyopita.

Katika mahojano maalum na idhaa hii muda mfupi baada ya kuhudhuria vikao hivyo, rais huyo mstaafu amesema idadi ya vijana inakuwa kwa kasi ambayo inaenda sambasamba na mahitaji yao ya msingi huku akitaka wahusishwe katika utatuzi wa changamoto hizo.

(SAUTI CHISSANO)

Hata hivyo Bwana Chissano amesema mahitaji ya msingi kwa wanawake ikiwamo afya ya uzazi pia ni changamoto inayopaswa kutiliwa mkazo.