Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mauaji ya wafanyakazi wawili wa UM

Ban alaani mauaji ya wafanyakazi wawili wa UM

Katibu Mkuu a Umoja wa Mataifa Ban Kin Moon amelaani vikali mauaji ya wafanyakazi wawili wa ofisi ya Mataifa ya kupambana na madawa ya kulevya na uhalifu UNODC katika uwanja wa ndege wa Galkayo Puntiland Somalia.

Katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya msemaji wa Katibu Mkuu mjini New York , Bwana Ban ametuma salamu za rambirambi kwa familia, marafiki na jamaa wa wahanga wa mauaji hayo.

Ametaka mamlaka husika kufanya uchunguzi wa kina kuhusu uhalifu huo na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria watekelezaji wake bila kuchelewa. Pia Bwana Ban ametoa shukrani zake kwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia kwa kujitoa kwao licha ya mazingira magumu na kuongeza kuwa umoja huo unaendelea kuunga mkono watu na serikali ya Somalia katika juhudi za kukuza amani, usalama na utawala wa sheria.