Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumepambana na malaria, kidinga popo kipo na juhudi zinaendelea: Tanzania

Tumepambana na malaria, kidinga popo kipo na juhudi zinaendelea: Tanzania

Leo dunia imeadhimisha siku ya afya, siku ambayo maudhui yake ni kutokomeza magonjwa yanayoambukizwa na wadudu mathalani malaria na homa ya denge yaani kidinga popo. Shirika la afya duniani WHO limetaka kutokomezwa kwa magonjwa hayo ambayo huathiri watu bilioni moja kote duniani na kuuwa milioni moja.

Nchini Tanzania taifa hilo linaelezwa kupiga hatua katika kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa malaria na magonjwa mengine lakini nchi hiyo inakabiliwa na mlipuko wa ugonjwa wa homa ya kidinga popo.

Serikali inachukua hatua gani wakati wa maadhimisho hayo ya siku ya afya? Dk Donald Mmbando ni mganga mkuu wa Tanzania na katika mahojinao na Joseph Msami wa idhaa hii anaeleza kampeni ya kutokomeza magonjwa yanayoambukiza na yale yasiyoambukiza.