Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwait yatoa dola milioni 100 kwa wakimbizi wa Syria

Kuwait yatoa dola milioni 100 kwa wakimbizi wa Syria

Serikali ya Kuwait imetangaza kuchangia dola milioni 100 kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, ili kusaidia wasyria.

Antonia Guterres, Mkurugenzi wa UNHCR, ameshukuru Kiongozi Mkuu wa Kuwait Sheikh Sabah Al-ahmed Al-Jaber Al-Sabah, pia serikali na wananchi wa Kuwait kwa mchango wao mkubwa. Aliongeza kwamba fedha hizo zinahitajika sana kwa kuokoa maisha ya wanaokimbia mzozo wa Syria, na pia kwa wakimbizi wa ndani.

Naamini kwamba kitu ambacho ni kipya katika msaada wa Kuwait, ni dira iliyowezesha serikali ya Kuwait kutambua jinsi ya kutumia mfumo wa usaidizi wa kibinadamu wa kimataifa unaweza kuongeza nguvu na ufanisi na kupaza sauti ya Kuwait kwa usaidizi wake wa kibinadamu Syria”.

UNHCR inahitaji dola bilioni 1.6 kwa ajili ya mzozo wa Syria na hadi sasa imepokea asilimia 22 tu ya kiwango hicho.