Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fukuto za tofauti katika jamii zishughulikiwe mapema kuepusha mauaji: Balozi Mulamula

Fukuto za tofauti katika jamii zishughulikiwe mapema kuepusha mauaji: Balozi Mulamula

Miaka 20 tangu kufanyika kwa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, ni vyema mataifa kuchukua hatua stahili na mapema pindi kunapoibuka fukuto za misingi mbali mbali ya tofauti katika jamii, amesema Balozi Liberata Mulamula, Katibu Mtendaji wa kwanza wa Mkutano wa kimataifa wa Maziwa Makuu, ICGLR.

Mulamula ambaye sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani amesema hayo katika mahojiano maalum na Idhaa hii.

(Sauti ya Balozi Mulamula )

Balozi Mulamula amesema mauaji ya kimbari yaliweka taswira mpya eneo la Maziwa Makuu na hivyo ICGLR ikapitisha mkataba wa kuhakikisha mauaji ya kimbari hayatokei tena, na hivyo waliunda kamati za kikanda na kitaifa ya kuepusha mauaji ya aina hiyo na mengine, na pindi kunapokuwepo na viashiria wakuu wa nchi hukutana mara moja.