Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Cambodia yatakiwa kuheshimu haki za binadamu

Cambodia yatakiwa kuheshimu haki za binadamu

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Cambodia Surya Subedi amelaani hatua ya hivi karibuni ya bunge la taifa hilo kukutana huku wabunge wa upinzani wakikosa fursa ya kushiriki.

Mjumbe huyo amesema kuwa kitendo cha bunge hilo kukutana kwa mara ya kwanza wiki iliyopita bila kuwepo kwa wabunge wa upinzani ni ishara mbaya na ameitaka Serikali ya Cambodia kumulika hali hiyo.

Amesema kuwa bado kumeendelea kujitokeza vitendo ambavyo vinabinya haki za binadamu jambo ambalo amesisitiza kuwa linakwenda kinyume na sheria za kimataifa.

Ametaka kutatuliwa kwa mikwamo ya kisiasa iliyojitokeza wakati wa uchaguzi uliopita wa mwaka 2013 na kusisitiza kwamba pande zote zinapaswa kushirikishwa kwenye mchakato wa ujenzi wa demokrasia mpya.