Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya wanachi CAR inazidi kuwa mbaya-UM

Hali ya wanachi CAR inazidi kuwa mbaya-UM

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameonya kuhusu kujitokeza kwa hali mbaya zaidi ikiwemo kuporomoka kwa hali ya uchumi kutokana na machafuko yanayoendelea katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Mashirika hayo lile la chakula na kilimo FAO na linalohusika na mpango wa chakula duniani WFP yamesema kuwa mkwamo unaoendelea kujitokeza nchi humo kumefanya mamia ya watu washindwe kumudu maisha yao ya kila siku.

Katika ripoti yao mashirika hayo yameeleza kuwa mamia ya watu wamepoteza mali zao ikiwemo kuharibika kwa shughuli za kilimo huku baadhi ya familia zikishindwa kuendelea na shughuli za kilimo jambo ambalo limewafanya wananchi hao kushindwa kujipata kipato cha kuendesha maisha yao.

Mashirika hayo yameweka shabaha ya kuzisaidia familia ikiwemo zile zilizokosa makazi kutokana na machafuko hayo