Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kujifunza pekee haitoshi, vitendo vyahitajika; Ban aieleza jamii ya kimataifa

Kujifunza pekee haitoshi, vitendo vyahitajika; Ban aieleza jamii ya kimataifa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amewasili Kigali nchini Rwanda tayari kushiriki kumbukizi ya miaka 20 tangu mauaji ya kimbari nchini humo ambapo amepongeza uongozi wa Rais Paul Kagame ulioitoa nchi hiyo katika hali ngumu hadi maendeleo ya sasa ya kiuchumi na kijamii.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mazungumzo yake na Rais Kagame, Bwana Ban amesema Rwanda imekuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingine kwani dunia imejifunza mengi kutoka nchi hiyo.

Hata hivyo amesema kujifunza pekee haitisho la muhimu ni kutekeleza somo kwa vitendo na hilo ndilo amejizatiti kutekeleza yeye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Bwana Ban amesema licha ya dunia kujifunza yaliyojiri Rwanda mwaka 1994 na Srebrenica mwaka 1995 bado kuna uwezekano wa viashiria kwingineko na ni lazima kuzuia mauaji ya kimbari na ukatili mwingine usiovumilika.