Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hukumu ya kifo ni ukiukwaji wa haki za binadamu, Somalia:OHCHR

Hukumu ya kifo ni ukiukwaji wa haki za binadamu, Somalia:OHCHR

Ofisi ya haki za binadamu ya umoja wa mataifa, OHCHR imepokea taarifa za kuuawa kwa mwanamume mmoja Aprili 3 mjini Kismayo , Somalia baada ya kutuhumiwa kumuua mzee mmoja mwezi uliopita. Mtuhumiwa alipatwa na hatia wiki iliyopita lakini haijulikani hukumu hiyo ilitolewa na nani na kuna uwezekano haikutolewa na mahakama.

Kulingana na taarifa ilizopokea ofisi hiyo mshtakiwa aliuwawa kwa kupigwa risasi hadharani Aprili 3. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia UNSOM ulikuwa umetoa wito wa kusitishwa kwa hukumu ya kifo kwa utawala wa muda wa Jubba ambao huenda walihusika kwa kiasi kikubwa katika hukumu na mauaji.

Rupert Colville ni msemaji wa ofisi hiyo.

OHCHR inasikitishwa na uamuzi huo wa haraka wa hukumu ya kifo kwani ilikuwa ni kwa kipindi cha siku tisa baada ya hukumu na  yeye kuuwawa. Hii ina maana kwamba hakupata fursa ya kuomba rufaa au uwakilishi wa kisheria kwani wakati watu wanahukumiwa wana haki ya kuomba rufaa. Kulingana na sheria za kimataifa hukumu ya kifo hutolewa baada ya mtu kushtakiwa mahakamani na kupewa fursa kujieleza kitu ambacho hakikufanyika katika kesi hii.”

Ameongeza kwamba kulingana na ripoti zaidi ya watu thelathini na wanne wamehukumiwa kifo tangu januari 2013 nchini Somalia.

OHCHR imetolea Somalia wito kurithia makubaliano ya kusitisha hukuma ya kifo waliosaini mjini Geneva 2011.