WFP kugawa fedha badala ya chakula Uganda

3 Aprili 2014

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Uganda litaanza kutoa pesa kwa wakimbizi badala ya chakula ili waweze kujinunulia chakula wanachotaka.

Mpango huo unawalenga  wakimbizi  ambao wameishi ukimbizini kwa muda mrefu. John Kibego wa radio wahsirika ya Spice FM,Ugandana taarifa kamili.

(Tarifa ya John KIibego)

Mpango huo utatekelezwa katika kambi za wakimbizi magharibi mwa Mto Nile na ile ya Kiryandongo ambako shirika limetathmini na kubaini uwezekano wake.

Lengo ni kuwapa fursa  wakimbizi hao kujinunulia chakula ambacho Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) halitoi.

Lakini watabaki na fursa ya kuchagua kati ya pesa na chakula, kama anayoeleza Lydia Wamala Msemaji wa shirikahilo nchini humo.

(Sauti ya Lydia Wamala)

WFP inapanga kutoa chaguo hiyo kwa wakimbizi ambao wameishi Uganda kwa muda mrefu, ambao wanapenda pesa badala ya chakula. Kwa sababu, kinawasaidia kupata chakula ambacho WFP haingewezi kuwapa. Kinapangwa kufanywa Magharibi ya Mto Nile na Kiryandongo”

Kumekuwepo tarifa za wakimbizi katika kambi mbali kuuza chakula cha WFP, ili wajinunulie chakula wanachotaka na kukudhi mahitaji mengine.