Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR kushirikiana na Uganda na DRC kurejesha wakimbizi makwao

UNHCR kushirikiana na Uganda na DRC kurejesha wakimbizi makwao

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kwa kushirikiana na serikali zaUgandana Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wanandaa kurejesha nyumbani takribani wakimbizi Laki moja na Elfu Themanini wa DRC walioko nchiniUganda.

Hatua hiyo inafuatia kifo cha wakimbizi 108 wa DRC waliozama katika Ziwa Albert wakati wajirejea nyumbani kivyao kutoka kambi moja nchiniUgandamwezi ulopita. John Kibego wa Radio washirika ya Spice FM, nchini humo araripoti kamili.

 (TARIFA YA JOHN KIBEGO)

Maafisa wakongwe kutoka DRC wakiwa na waziri wa kushughulikia majanga  na wakimbizi wa Uganda Hllary Onek, wamtemlbelea kambi ya Kyangwali mlimo toroka wakimbizi waliozama Ziwani.

Waziri Onek alisema,

 (Sauti ya Hillay Onek)

Ujumbe wa maafisa saba wa DRC wakiwemo waziri wa mambo ya ndani Richard Moyenz na waziri mdogo wa mambo ya nje  Tunda ya Kasende waliongozwa na balozi wao nchini Uganda Jean Charles Okoto.

Balozi Okoto aliwataka wakimbizi wawe na subra kwani tayari amani imerejea kwao.

 (Sauti ya Jean Charles Okoto)

Naibu mwakilishi wa UNHCR nchini Uganda Sakua Atsumi alisema kwamba sala yake ni kuona kwamba wakimbizi hao wamaishi salama na kurejea nyumbani wakiwa salama.

(Sauti ya Sakura Atsumi)