Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wote ni wazee watarajiwa: Kamishna ustawi wa jamii Tanzania

Wote ni wazee watarajiwa: Kamishna ustawi wa jamii Tanzania

Ikiwa jukwaa la kijamiii la haki za binadamu linakutana mjini Geneva katika mkutano wa siku tatu ambao utalenga kujadili haki za wazee ikiwemo mifumo kuhusu kundi hili watetezi wa haki za wazee wanasema

Ni muhimu kundi hilo litahiminiwe.

Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa kamishna mkuu wa ustai wa jamii nchini Tanzabia Dunford Makala amesema

ni lazima kila mtu kwa nafasi yake akumbuke iko siku atakuwa mzee akitoleas mfano yey mwenyewe ambaye kwa mujibu wa sheria za nchi yake amebakiza mwaka mmoja kuingia rasmi katika kundi hilo.

Bwana Makala kwanza anaanza kwa kueleza idara ya ustawi wa jamii nchini humo inafanya nini katika kutoa kipaumbele kwa wazee

(SAUTI MAHOJIANO)

Mkutano huo wa Geneva utakao kamilika April 3 ni mfululizo wa mikutano ya ofisi ya haki za binadmu katika Umoja wa Mataifa ambayo inaangazia haki hizo katika ngazi mbalimbali.