Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jukwaa la kijamii la haki za binadamu kukutana Geneva

Jukwaa la kijamii la haki za binadamu kukutana Geneva

Jukwaa la kijamiii la haki za binadamu linakutana mjini Geneva katika mkutano wa siku tatu ambao utalenga kujadili haki za wazee ikiwemo mifumo kuhusu kundi hili.

Jukwaa hili la kijamii ambalo hukutana mara moja kwa mwaka huendesha mijadala ya wazi inayoleta pamoja wawakilishi wa serikali , asasi za kiraia ikiwamo mashirika kutoka mashinani na asasi za kiserikali ambapo mijadala ya ya kitaifa na kimataifa juu ya namna ya kukuza haki za binadamu hupewa kipaumbele.

Kikao hiki ni mfululizo wa mikutano ya ofisi ya haki  za binadamu katika Umoja wa Mataifa ambayo inaangazia haki hizo katika ngazi mbalimbali.