Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sasa tugeukie vitendo ili kusaidia watu wenye ulemavu wa akili: Kongamano

Sasa tugeukie vitendo ili kusaidia watu wenye ulemavu wa akili: Kongamano

Wakati dunia ikijiandaa kuadhimisha siku ya kuelimisha umma kuhusu matatizo ya ulemavu wa akili au Autism Aprili pili , hii leo kumefanyika kwenye Umoja wa Mataifa kikao cha ngazi ya juu kubadili uhamasishaji kuhusu ugonjwa huo kuwa vitendo.

Kabla ya kuwasilishwa mada mbali mbali, video yenye ujumbe wa watoto na Katibu Mkuu Ban Ki-Moon ilichezwa ikionyesha vile ambavyo wanataka kuzingatiwa kwa mahitaji ya kiuchumi na kijamii ya wagonjwa bila kusahau familia zao. Mahitaji yao ni pamoja na elimu, afya na ajira.

Nigeria ni moja ya waratibu wa kongamano hilo na kupitia Naibu mwakilishi wake wa kudumu kwenye Umoja wa Mataifa, Balozi Usmani Sarki ikasema vitendo sasa vimeanza.

(Sauti ya Balozi Usmani)

“Sheria kuhusu ubaguzi dhidi ya watu wenye ulemavu imeanza kutumika mwaka huu na tutaunda tume ya watu wenye ulemavu ili suala la kupatia umuhimu ulemavu wa akili litafikishwa kwenye ngazi ya kipekee ili liwe ajenda ya kitaifa.

Ulemavu wa akili ni tatizo la kiafya linalojitokeza katika miaka mitatu ya kwanza utotoni na mwaka 2007, Umoja wa Mataifa ulitambua Aprili Pili kuwa siku ya kuhamasisha.