Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNDP yazindua mkakati wa kuwezesha vijana katika maendeleo

UNDP yazindua mkakati wa kuwezesha vijana katika maendeleo

Shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP, limezindua kongamano la siku tatu kuhusu vijana na maendeleo, huku Tunisia likisema kuwa licha ya kwamba vijana, ndio wanaokabiliwa zaidi na umaskini na shida za kiuchumi, afya au ghasia bado wana umuhimu mkubwa katika kujenga maisha endelevu kwa baadaye.

Mkutano huo ni sehemu ya maandalizi ya ajenda ya maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015 ambapo UNDP inakusanya maoni ya vijana ambao wamerejelea maombi yao kushirikishwa zaidi katika mambo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, na kusikilizwa zaidi.

Kwa hiyo, UNDP limeanzisha mkakati wa vijana ili kuwawezesha kushirikiama zaidi kufikisha maendeleo endelevu.

Msemaji wa UNDP, Sima Bahous, amesema kwamba bado vijana wengi wanakata tamaa, kwa sababu hawana elimu ya kutosha, pia hawana kazi au hawafaidiki na kazi zao,na wala hawana fursa za kushirikiana katika maamuzi yanayowahusu… Aliongeza kwamba inabidi vijana watuonyeshe maisha wanaotaka kwa baadaye kwa watoto wao, wajukuu wao, na watakaokuja baadaye.

(Sauti ya Bahous )

“ Mkakati wa UNDP unazingatia nguzo tatu muhimu. Nguzo ya kwanza inalenga ushiriki na uwezeshaji wa vijana kwenye mambo ya kiuchumi, ya pili inaangazia ushiriki wa vijana katika maswali ya kisiasa na utawala bora, na ya tatu inaangalia jinsi ya kusaidia vijana kupona baada ya vita au mizozo”