Tunaunga mkono hatua ya maridhiano na uundwaji wa serikali Somalia: UM

31 Machi 2014

Mwakishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Nicholas Kay, amekaribisha ziara ya rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud kukutana na wafuasi wanaopinga mchakato wa kuundwa kwa serikali.

Taarifa iliyotolewa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNSOM imemkariri balozi Kay akisema kuwa UNSOM itaendelea kuunga mkono maridhiano kati ya serikali yaSomalia, wanasiasa na  viongozi wa dini huko Baidoa.

Amesema ziara hiyo muhimu inasisitiza jukumu la serikali ya shirikisho la kuimarisha amani na utulivu katika ukanda huo na kuongea kuwa ni muhimu pande zote kufanya kazi kwa pamoja na serikali kutafuta amani na suluhisho jumuishi na kuepusha vitedno ambavyo vyaweza kuhatarisha la usalama ua kudhoofisha utulivu.

Mwakailishi huyo maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema UNSOM itaendelea kufanya kazi na wabia wa kimataifa mathalani ujumbe wa muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM, na shirika la kimataifa la maendeleo IGAD kufanikisha maridhiano na mchakato wa kuunda serikali chini ya serikali ya shirikisgho la Somalia.

Wiki iliyopita serikali ya shirikisho laSomalia ilitaka mashauriano ya dharura na wanasiasa na viongozi wa kidini huko Bidoa ili kupunguza mvutano kati ya wafuasi wa muundo tofauti wa serikali katika ukanda huo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter