Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi hazikwepeki: UM

Hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi hazikwepeki: UM

Jopo la kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, IPCC linalokutana huko Yokohama Japan limezindua ripoti yake ya tathmini na kueleza kuwa madhara ya mabadiliko hayo ni dhahiri kwenye mabara yote duniani na yanaweza kuwa mabaya zaidi na yasiweze kurekebishika iwapo hatua hazitachukuliwa. Taarifa zaidi na George Njogopa.

(Taarifa ya George)

Ripoti hiyo imeelezea kile ilichokiita fursa zinazoweza kutumika ili kukabiliana na tishio hilo la mabadiliko ya tabia nchi, lakini imesisitiza kuwa bado itakuwa ni vigumu kudhibiti athari hizo hasa kutokana na kuendelea kuongezeka kwa hali ya ujoto.

Ripoti hiyo yenye kichwa cha habari kisemacho mabaidliko ya tabia nchi mwaka 2014, imeandikwa na jopo la wataalamu 309 kutoka mataifa 70.

Akizungumzia kuhusu ripoti hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNEP Achim Steiner alisema kuwa kwa kuzingatia ripoti hiyo binadamu unahusika moja kwa moja.

Amesema kuwa shughuli za binadamu zinachangia kwa sehemu kubwa mabadiliko yanayojitokeza sasa.

Katika kuangazia zaidi hatua za kuchukua kudhibiti na kupunguza madhara ya mabadiliko ya tabianchi duniani, Chris Field ambaye ni mwenyekiti mwenza wa kikundi kazi cha IPCC anasema..

(Sauti ya Chris)