Japan yatakiwa kusitisha uvuvi wa nyangumi huku Antarctic

31 Machi 2014

Mahakama ya haki ya kimataifa ya haki, ICJ leo imetangaza kuwa uvuvi unaofanywa na Japan kwenye eneo la Antarctic ni kinyume na mkataba wa kimataifa na hivyo kutakiwa kusitisha mara moja.

Uamuzi huo umetangazwa na Jaji Peter Tomka wakati akisoma hukumu ya kesi iliyofunguliwa na Australia dhidi ya Japan mwezi Mei 2010 ikipinga madai ya Japan kuwa uvuvi wa nyangumi kwenye eneo hilo ni kwa minajili ya utafiti wa kisayansi.

Jaji Tomka amesema kura 12 kati ya Nne zimepitisha uamuzi huo akieleza kuwa imethibitishwa pasipo shaka kwamba uvuvi ulikuwa na viashiria vya utafiti lakini havikutosheleza kuwezesha mahakama kutupilia mbali kesi hiyo.

Mathalani amesema licha ya Japan kupatiwa kibali maalum cha kuua na kuchukua nyangumi, nchi hiyo haikuwajibika kwa mujibu wa mkataba wa kimataifa wa kudhibiti uvuvi wa nyangumi.

(Sauti ya Jaji Tomka)

ICJ imesema tangu Japan ianza mradi wake mwaka 2005 imevua nyangumi 3,600 lakini kiwango cha utafiti wake kisayansi kimekuwa na ukomo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud