Umoja wa Mataifa kushiriki zoezi la kuzima taa kuhifadhi nishati

29 Machi 2014

Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wameombwa kuzima taa kwa saa moja siku ya jumamosi tarehe 29 March 2014 katika tukio lililopewa jina ‘muda wa dunia 2014’ ikiwa ni juhudi za kimataifa ambapo mamilioni ya watu, makampuni na taasisi mbalimbali pamoja na serikali zinashiriki pamoja katika kuzima taa kwa saa moja ikiwa ni ishara ya kuhifadhi nishati.

Hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa taa zitazimwa kwa saa tatu kuanzia saa moja jioni hadi saa nne usiku, zoezi litakalosimamiwa na kaimu katibu mkuu Jan Eliasson.

Pia Umoja wa Mataifa umetaka wafanyakazi wake kuungana na watu wengine katika zoezi hilo muhimu kwa kuhakikisha kuwa wanazima taa majumbani kwao kwa angalau saa moja. Imeelezwa kuwa kufanya hivyo kutasaidia katika juhudi za pamoja za kupambana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanapigiwa upatu na UM na jumuiya ya kimataifa.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud