Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marufuku ya matumizi ya mtandao ni ukiukwaji wa haki msingi Uturuki

Marufuku ya matumizi ya mtandao ni ukiukwaji wa haki msingi Uturuki

Mtaalamu huru wa haki wa Umoja wa Mataifa amesema kwamba uzuiaji wa mtandao wa kijamii na serikali ya Uturuki ni ukiukwaji wa haki za watu wa Uturuki.

Serikali imewazuia kutembelea mitandaokamaYou tube na Twitter huku uchaguzi ukitarajiwa kufanyika Jumapili, licha ya marufuku dhidi ya matumizi ya Twitter kuondolewa na mahakama.

Habari kuhusu maandamanaji dhidi ya serikali ambayo yalipangwa na kutangazwa kupitia mtandao wa kijamii zilichukua nafasi kubwa mwaka jana.

Mtaalamu huyo maalum kwa ajili ya haki ya kujieleza, Frank La Rue amesema kwamba shauku kuhusu usalama wa taifa ni halisi.

Lakini ameongeza kuwa kupiga matumizi ya mtandao marufuku unakiuka haki msingi ya kujieleza.