Kituo cha teknolojia kukuza ajira na upatikanaji wa nishati Ethiopia

28 Machi 2014

Kituo cha kukuza makampuni chipukizi ya teknolojia safi ambayo inashughulikia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na kuongeza ajira kimezinduliwa mjini Adis Ababa Ethipoia.

Kituo hicho cha ubunifu katika masuala ya hali ya hewa nchini humo kinachofadhiliwa na bank ya dunia kinatarajiwa kusaidia zaidi ya raia milioni 3 nchiniEthiopiakatika kuendana na mabadiliko ya tabia nchi

Teknolojia hiyo ya kisasa inayomilikishwa kwa wajasiriamali wazalendo inatarajiwa kuongeza uapatikanaji wa nishati kwa watu zaidi ya laki mbili.

Kadhalika teknolojia hiyo ianatarajiwa kuongeza ufanisi wa kilimo kwa kuinua zaidi ya wakulima laki moja.Wataalamu wanakisia kuwa pasipo na mkakati wa kukuza uchumi unaozingatia mazingira,  mabadiliko ya tabia nchi yanaweza kuigarimu Ethiopia zaidi ya  dola bilioni 5 kwa mwaka

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud