Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati ya kuchunguza uvamizi wa ardhi Uganda yakamilisha kazi

Kamati ya kuchunguza uvamizi wa ardhi Uganda yakamilisha kazi

Nchini Uganda, kamati iliyoundwa kuchunguza wavamizi na kufungwa mpaka wa ardhi ya wakimbizi ya Kyangwali imemaliza kazi yake na kubaini kuwa takribani watu 15,856 wanaishi kwenye ardhi hiyo.

Hatua hiyo ilichukuliwa kufuatia mzozo wa ardhi ya kambi hiyo uliosababisha maelfu ya wakimbizi kuhamishwa hadi kwenye kambi nyingine mwaka jana.

Tarifa kamili na John Kibego wa Radio washirika ya Spice FM, nchini humo.

Hi leo Maj. Gen. Julius Oketa mwenyekiti wa kamati hiyo amelieleza baraza la wilaya husika ya Hoima tarifa muhimu kuhusu ripoti ya uchunguzi uliofanywa kwanzia mwezi Oktoba mwaka uliopita.

Amesema, sasa kazi imekamilika na kinachofuata ni kuipeleka repoti hiyo mbele ya baraza la mawaziri watie sahihi ndiyo hatua ichukuliwe.

(Sauti ya Maj. Gen. Julius Oketa)

Amesema, kuna makundi manne wakiwemo wafugaji wa kuhamahama na wale wenye hati miliki za ardhi kwenye ardhi ya serkali. Kwa mujibu wake, wote wenye hati miliki za ardhi wataanza kukabiliwa kisheria.

(Sauti ya Maj. Gen. Oketa)

Kuna zaidi ya wakimbizi 30,000 kwenye ardhi hiyo yenye ukubwa wa maili 56 mraba.