Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya usalama nchini CAR bado ni tete:UNHCR

Hali ya usalama nchini CAR bado ni tete:UNHCR

Shrika la kuhudumia wakimbizi katika Umoja wa Mataifa UNHCR, limesema kwamba hali ya usalama Bangui nchini Jamhuri ya Afrika ya kat ni dhaifu kwani chuki dhidi ya jamii ya waislamu ni ya juu. Maelfu ya waislamu wamenaswa eneo la Borda.

Mkurugenzi wa kitengo cha usalama wa kimataifa UNHCR Volker Turk ambaye alikuwa nchini CAR kutathmini hali halisi, amesema kwamba kungalikuwa na mauaji ya kimbari iwapo jeshi la Ufaransa lisingalikuwepo kwani waasi wa Balaka wanaendelea kujihami

(SAUTI TURK)

Mjini Bangui tulikuwa tunaona waasi wa Anti-balaka wakizunguka zunguka kwa njia isiyotabirika na hatari. Tulishuhudia ukatili barabarani. Kiwango cha uwoga na kiwewe miongoni mwa jamii ni cha juu. Uwoga pamoja na maswala ya kidini yanatumika kama nyenzo za uhasama.”

Ameogeza kwamba serikali haina uwezo wa kukabiliana na hali hii na mashirika ya misaada hayawezi kuchukua jukumu la kutoa ulinzi. Ametolea wito jamii ya kimataifa kuingilia kati.

Nalo shirika la kutoa misaada ya kibinadamu OCHA limesema kwamba wakati CAR ikiadhimisha kutwaliwa kwa utawala na kundi lililojiita Seleka, ghasia zimekatiza uwasilishaji wa misaada ya kibinadamu na wakimbizi wa ndani wameongezeka kutoka 177,000 hadi 200,000 huku watu 18 wakiuwaa katika kipindi cha siku moja.