Watoto wazidi kuteseka Sudani Kusini: UNICEF

28 Machi 2014

Siku mia moja tangu kuzuka kwa mzozo nchini Sudani Kusini, watoto ndio waaathiria wakuu kutokana na machafuko na kukosa makazi kunakozidi kuwakumba raia nchini humo, liomesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Akiongea mjini Geneva msemaji wa shirika hilo Sarah Crowe amesema hali ya watoto nchini Sudani Kusini inatarajiwa kuwa mabaya zaidi wakati huu ambapo mzimu wa mvua unatarajiwa kuanza, hatua ambayo itafanya zoezi la kuwafikishia misaada waathiriwa kukwama.

( SAUTI SARAH)

UNICEF inasema takribani watu milioni moja watakbiliwa na uhaba wa chakula.

Wakati huo huo shirika la la mpango wa chakula duniani WFP limeanza operesheni ya dharura ya kufikisha vyakula, chanjo na virutubisho katika moja ya maeneo ya pembezoni yalioathiriwa na mzozo nchini Sudan Kusini kwa kutumia ndege na vifaa maalum vya kudondosha vifurushi kutoka angani.

WFP kwa kushirikiana na UNICEF wanasaidia watu elfu 30 wanaohitaji misaadaya dharura katika jimbo la Jonglei karibu na mpaka wa Ethiopia. Mashirika hayo mawili yameweka vituo vaa ugawaaji wa vyakula, huduma za afya, ulinzi, elimu na huduma za kujisafi

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud