Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lapitisha azimio la kuongeza muda wa MONUSCO

Baraza la Usalama lapitisha azimio la kuongeza muda wa MONUSCO

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo kwa kauli moja limepiga kura kupitisha azimio la kuongeza muda wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC na vikosi vya kujibu mashambulizi dhidi ya makundi yenye silaha mashariki mwa nchi hiyo, hadi tarehe 31 Machi mwaka 2015.

Katika azimio hilo, Baraza la Usalama limelaani makundi yote yenye silaha yaliyopo kwenye ukanda wa Maziwa Makuu na ukiukwaji wa haki za kibinadamu za kimataifa, uvunjaji wa haki za binadamu, ukiwemo kuwashambulia raia, walinzi wa amani wa MONUSCO na wahudumu wa kibinadamu, pamoja na mauaji ya kiholela, ubakaji na ukatili mwingine wa kijinsia pamoja na kuwaingiza watoto katika mapigano.

Baraza la Usalama pia limeyataka makundi ya FDLR, ADF, LRA, Bakata-Katanga na Mayi Mayi kukomesha mara moja aina zote za machafuko na vitendo vingine vinavyoathiri utulivu, na kuwataka wafuasi wa makundi hayo kujisalimisha mara moja na kuwaondoa watoto katika vikosi vyao.

Akizungumza baada ya kupitishwa azimio hilo, Mwakilishi wa Kudumu wa DRC, kwenye Umoja wa Mataifa, Atoki Ileka amelishukuru Baraza la Usalama wa kwa azimio hil

SAUTI YA ILEKA

Baadaye Baraza hilo linatarajiwa kufanya mazungumzo kuhusu Syria, ambapo pia litasikiliza ripoti kuhusu hali ya kibinadamu nchini humo.