Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afghanistan yasifiwa kwa maandalizi ya uchaguzi

Afghanistan yasifiwa kwa maandalizi ya uchaguzi

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Mkuu wa Operesheni za Ulinzi wa Amani katika Umoja wa Mataifa,

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

Hervé Ladsous, amesema Umoja wa Mataifa unashikamana na watu wa Afghanistan wakati huu muhumu wanapoenda kwenye uchaguzi wa urais na viongozi wa mabaraza ya mikoa. Bwana Ladsous amesema Umoja wa Mataifa unawaunga mkono raia wengi wa Afghanistan, ambao wanatarajia kupiga kura, akiongeza kuwa ni muhimu kwa kila mtu anayefuzu kupiga kura akafurahia haki yake ya kupiga kura, na kutoa kauli yake katika kuamua mustakhbali wa taifa. Amesema uchaguzi wa Afghanistan unapaswa kuendeshwa na watu wa Afghanistan wenyewe

“Uendeshwe na Waafghanistani, na umilikiwe na Waafghanistani. Unahusu kuwawezesha watu kuwachagua viongozi wao wenyewe. Na kwetu kama Umoja wa Mataifa, unahusu kutoegemea upande wowote. Umoja wa Mataifa haumuungi mkono mgombea yeyote dhidi ya mwingine. Ni raia wa Afghanistan wenyewe ndio wanaandaa uchaguzi. Sisi tupo hapa tu kutoa msaada wa kitaalam kwa mamlaka za uchaguzi za Afghanistan.”

Bwana Ladsous amesema amefurahi kuona kuwa, ukilinganishwa na uchaguzi uliopita, maandalizi ya sasa yanaonyesha kuboreshwa kwa hali.

“Nimefurahi pia kuona kuwa juhudi zimefanywa kuwawezesha wapiga kura kupiga kura zao kwa usalama, na hatua zimechukuliwa hususan kwa ajili ya kuboresha mazingira ya usalama. Kweli, hilo ni jambo la kupongezwa.”

Ladsous ameongeza kuwa, kwa mtazamo wa Umoja wa Mataifa, wanawake wana mchango mkubwa katika uchaguzi huo, siyo tu kama wapiga kura, lakini pia kama wagombea na pia kama maafisa wa uchaguzi. Amesema bila wanawake kushiriki, kura hiyo haiwezi kuwa wakilishi na ya kuaminika.