Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jeshi la Somalia laendesha operesheni ya kuwasaka Al shabaab

Jeshi la Somalia laendesha operesheni ya kuwasaka Al shabaab

Mfululizo wa matukio ya kigaidi yameendelea kuripotiwa nchini Somalia likiwemo la hivi karibuni zaidi ambapo wazee wa nane wa koo nchini humo waliuwawa huku kundi la kigaidi la Al shabaab likikiri kuhusika katika tukio hilo.

Jeshi la Somalia kwa kushirikiana na vikosi vya muungano wa Afrika AMISOM liko katika operesheni kali ya kutokomeza mtandao wa kundi hilo. Ungana na Joseph Msami katika makala ifuatayo.