Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu aonya haki bila upendeleo ndiyo mwarobaini wa Cote d’Ivoire

Mtaalamu aonya haki bila upendeleo ndiyo mwarobaini wa Cote d’Ivoire

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Cote d’Ivoire Doudou Diène ameelezea kusikitishwa kwake na kile alichokiita kutokamilika kwa mchakato wa taifa wa maridhiano nchini humo inapoelekea uchaguzi mkuu mwaka 2015.

Bwana Diène amesisistiza kuwa ni muhimu kuwepo na haki bila upendeleo kwa wote katika nchi ambayo ilikumbwa na sintofahamu baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 . Ameonya kuwa hadi sasa ni watu kutoka upande wa rais wa zamani wa nchi hiyo Laurent Gbagbo pekee ndio wanatuhumiwa kwa uhalifu na kuwekwa gerezani.

(SAUTI DOUDOU)

Ametoa wito wa kuharakishwa kwa kesi inayomkabili mke wa raisi wa zamani wa Cote d’Ivoire Gbagbo. Bwana Gbagbo anakabiliwa na mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC.