Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICTR kukamalisha kazi zake mwakani

ICTR kukamalisha kazi zake mwakani

Pamoja na kukumbuka miaka ishirini ya mauaji ya kimbari Rwanda, Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu nchini humo, ICTR, inafikia miaka ishirini ya kazi zake na kutarajia kukamilisha majukumu yake. Priscilla Lecomte na ripoti kamili.

(Taarifa ya Priscilla )

Wakizungumza mbele ya waandishi wa habari, Msaidizi wa Katibu Mkuu na Msajili wa ICTR, Bwana Bongani Majola, na Mshauri wa Kisheria wa Msajili ICTR, Daktari Ousman Njikam, wamesema ICTR, ilitakiwa kumaliza kazi zake mwaka huu kwa mamlaka ya Umoja wa Mataifa. Hata hivyo kutokana na kesi tano za rufaa zilizobaki kusikilizwa, mahakama inatarajia kukamilisha kazi zake Septemba mwaka ujao 2015.

Kwa mujibu wa Bwana Majola, baada ya kupewa majukumu yake na Umoja wa Mataifa, mahakama ya ICTR ililenga kesi za watu walioshirikiana katika kupanga na kuchukua maamuzi ya mauaji ya kimbari kwa ngazi ya kitaifa.

Kwa jumla, mahakama ilifanikiwa kutiwa hatiani watu 62, watu wengine 14 wakiachiliwa. Bwana Majola aliongeza kwamba mahakama ilikabiliana na changamoto nyingi, zikiwemo kupata ushirikiano mzuri na nchi kwa ajili ya kusaka washtakiwa, na kupata mashahidi