Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mikakati ya maendeleo yapigwa jeki Kenya:UNDAF

Mikakati ya maendeleo yapigwa jeki Kenya:UNDAF

Umoja wa mataifa na Serikali ya Kenya zimetia saini mkataba wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya mikakati ya maendeleo UNDAF, ambapo Kenya itapokea Shilingi Bilioni 102 kwa ajili ya mikakati ya maendeleo kwa kipindi cha miaka minne.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliofanyika Ikulu mjini Nairobi Kenya, Mwakilishi mkaazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo Nardos Beleke Thomas amesema kwamba wameshawishiwa na maono ya Serikali ya kuja pamoja na kutekeleza wajibu kwa pamoja.

(Sauti ya Nardos)

Kwa upande wake Rais Uhuru Kenyatta akipokea ujumbe huo amesema kwamba usaidizi huo utachangia katika kutekeleza baadhi ya mikakati ya Serikali.Ikiwemo mambo manne muhimu.

(Sauti ya Kenyatta)