Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waonya kuzorota kwa usalama CAR

UM waonya kuzorota kwa usalama CAR

Jamhuri ya Afika ya Kati inapewa fursa ya mwisho kukomesha machafuko , ameonya Babakar Gaye, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu nchini humo. Akizungumza na waandishi wa habari siku ya leo, Bwana Gaye amelaani mashambulizi yaliyotokea dhidi ya wanajeshi walinda amani  na vitisho vya vifo kwa wafanyakazi wa umoja wa mataifa kwa misingi ya imani za kidini.

Alitoa wito kwa vikosi vya pande zote kusitisha mapigano na kwa viongozi wote kufikia maridhiano.

“ Tunashuhudia kuzorota kwa hali ya usalama na ya kijamii nchini humo. Kuna watu walioshambuliwa mjini katikati, bila sababu yeyote, isipokuwa ya kuonekana kama wafuasi wa dini fulani.  Nchi hiyo inaelekea kusambaratika, na haitaepukana na hali hiyo, kama hatua hazichukuliwi kwa ngazi ya kitaifa. Inabidi wimbi la machafuko likomeshwe”.

Kuhusu jinsi ya kusitisha mzozo huu, Bi Marie-Thérèse Keita Bocoum ambaye ni Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa, alisema kwamba ni muhimu kuwezesha serikali na mahakama ili ziweze kulinda amani. Alionya kwamba bado mauaji ya kidini yanaendelea, na haki za kidinadamu zinaendelea kutoheshimiwa. Akitoa repoti yake mbele ya Kamisheni ya Haki za Kibinadamu, alisisitiza kwamba, licha ya mvutano wa kidini, asili ya ghasia za CAR zinatokea na udhaifu wa serikali na taasisi zake katika kuleta maendeleo kwa watu wote nchini humo.

“Kitu cha muhimu hivi sasa, jinsi nilivyosema, ni kufikiria sababu za awali ya mzozo huo, yaani, ni kuangalia usalama wa nchi na kuangalia utawala bora, pia, kurudisha nguvu za serikali na taasisi zake, ili zitimize majukumu yao ndani ya nchi na kwa mashirika ya kimataifa. Ni muhimu serikakli iweze kutimiza jukumu lake la kulinda wananchi wake. Hii ndiyo maana ya uhuru”