Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vietnam yaombwa isitishe kuwafukuza wakaazi

Vietnam yaombwa isitishe kuwafukuza wakaazi

Wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za bindamu wametolea wito serikali yaVietnam kuingilia kati na kusitisha shughuli za kuwafukuza wakaazi wa kijiji kidogo katikati mwa nchi.

Wakaazi wa kijiji hicho kilichoko nje kidogo mwa mji waDa Nangni moja ya nyumba takriban 100 ambapo wakaazi wameamrishwa kuondoka au makaaziyaoyabomolewe.

Wataalam hao wamesema kuwa ufukuzaji huo ni uporaji wa ardhi unaonuia kuwanufaisha watu binafsi huku wenyeji ambao hawajapewa fidia ya kutosha wakisahaulika, na makaazi mbadala yakiwa maeneo ya mbali.

Wametolea mfano wa 2007 ambapo Serikali za mitaa yaDa Nangiliamua kuchukua ardhi katika kijiji cha Con Dau na kukodisha kwa kampuni binafsi ya Sun Land kwa ujenzi wa sehemu ya mapumziko.

Wakaazi ambao walikuwa wakitumia ardhi kwa ajili ya makaazi na kilimo, na ambao waliupinga mradi huo, walishurutishwa kuhama mwaka 2013 baada  ya kutishiwa huku wengine wakishuhudia nyumba zao zikibomolewa.

Mapema mwezi huu wakaazi walipewa ilani ya Aprili 15 kuhama.

Kwa sasa uharibifu wa makaazi unaendelea na wataalamu wanaonya kwamba huenda nyumba zote zikaharibiwa kabla ya kufikia siku hiyo.